Alhamisi, 2 Desemba 2021

ROHO WA MUNGU. (wimbo)

(1) Roho wa Mungu hudhuria Maombi yetu Shuka Kwa nguvu zako zote za Neema Utuongoze katika njia ya uzima tawala ndan yetu ishi ndani yetu,Ee Roho mkuu njoo.

Njoo kwetu kama Nuru utuongoze.
Njoo kwetu kama Moto, utakase mioyo yetu
Njoo kwetu kama njiwa utandaze mbawa zako, mbawa za upendo na Amani, Kanisa lako libarikiwe.

(2) Roho wa Mungu ,usikie Maombi yetu, Shuka Kwa nguvu zako zote za Neema uwafariji waliokosa tumaini, uwe karibu nao uwatie nguvu, Ee Roho mkuu njoo.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni