Alhamisi, 2 Desemba 2021

KAMA NINGALIWEZA (wimbo)

(1) Kama ningali weza kuja kila siku, kukaribia karibu na Mungu wangu, hata mawazo yangu yangeelekea katika Neno lako nikutumikie. Naja kwako Bwana niwezeshe, nipe Roho wako Bwana nikutumikie.Naja kama nilivyo najitoa kwako, nitakase niweze kukutumikia.

Mungu wangu najitoa kwako, ninajua hutanikataa, nisamehe dhambi niwe mkamilifu kwako, niwe sehemu ya familia ya Mbinguni.

(2) Uwe kwangu majibu kwa maswali yangu, ninapokuhitaji nikuone Yesu, wewe ni msaada ulio karibu nione uso wako nipate neema. Ishi ndani yangu siku zote , palipo na mashaka ulete majibu, faraja na neema ziwe nami Bwana, ukae nami Bwana siku zangu zote.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni