Jumatano, 8 Desemba 2021

YERUSALEMU MAKAO YANGU

(1)Yerusalemu makao yangu, yenye furaha na amani tele, O, jinsi ninavyokutamani, kupa ingia pale. huzuni zangu zitaisha lini, furaha nitaziona lini? Nikifika nyumbani Kwa Baba hapo nitapata pumziko.

Yesu tusaidie Kwa Neema yako kuu, ili tuendelee kukungojea, mpaka utakaporudi kutuchukua kwenye makao yaliyo barikiwa.

(2)Yerusalemu ni nchi tamu, yenye baraka na Amani tele. Nchi ya wateule wa Mungu, walio shinda dhambi Mioyo yenye shauku kubwa, inatarajia kuja kwako Bwana, Yesu twakuomba tupeleke Nchi pendwa ya mapumnziko.


Alhamisi, 2 Desemba 2021

BWANA KIMBILIO LANGU (wimbo)

(1) Bwana kimbilio langu tena ndiye msaada wangu, ni ngome yangu ndiye wokovu wangu msaada ulio karibu

Sasa najua ya kwamba sioni cha kunitenga naye, iwe ni shida, iwe ni njaa, siwezi tengwa naye

(2) Bwana mchungaji wangu tena ndiye kiongozi wangu, yeye ni mwamba wa wokovu wangu, sina hofu na kitu chochote

(3) Bwana mkombozi wangu tena ndiye mlinzii wangu, ni mwogope nani, sina chakuogopa kwani Yesu rafiki wa kweli.


NIMEAMUA KUISHI NDANI YA YESU ( wimbo)

(1)Nimeamua kuishi ndani ya Yesu, naku achana na mambo ya dunia hii, sijaona faida ya kuipenda dunia niheri, niheri kuishi na Mwokozi.

Tangu sasa mtu asinitaabishe, mwilini mwangu naibeba chapa ya Yesu, yeye ndani yangu, Mimi ndani yake nitamwandama daima,

(2) Ee ndugu yangu utulie Kwa Yesu hapo ndipo lilipo tumaini lako, huna sababu yaku hangaika naya dunia, tulia, tulia, tulia kwa Mwokozi.


KAMA NINGALIWEZA (wimbo)

(1) Kama ningali weza kuja kila siku, kukaribia karibu na Mungu wangu, hata mawazo yangu yangeelekea katika Neno lako nikutumikie. Naja kwako Bwana niwezeshe, nipe Roho wako Bwana nikutumikie.Naja kama nilivyo najitoa kwako, nitakase niweze kukutumikia.

Mungu wangu najitoa kwako, ninajua hutanikataa, nisamehe dhambi niwe mkamilifu kwako, niwe sehemu ya familia ya Mbinguni.

(2) Uwe kwangu majibu kwa maswali yangu, ninapokuhitaji nikuone Yesu, wewe ni msaada ulio karibu nione uso wako nipate neema. Ishi ndani yangu siku zote , palipo na mashaka ulete majibu, faraja na neema ziwe nami Bwana, ukae nami Bwana siku zangu zote.