Alhamisi, 18 Juni 2015

UPONYAJI WA MUNGU KUPITIA MAOMBI:

Kristo ni tabibu yule yule mwenye huruma sasa kama alivyokuwa wakati wa kazi zake hapa duniani. Ndani yake kuna zeri iponyayo kwa kila udhaifu wa mwili. Wanafunzi wake wa siku hizi wanatakiwa kuwaombea wagonjwa kama vile wanafunzi wa zamani wakivyowaombea. Uponyaji utafuata; kwakuwa kule kuomba kwa imani kutamuokoa mgonjwa yule" (Yakobo 5:14-15). Alipokuwa hapa duniani, Yesu alifundisha ya kwamba imani ni sehemu muhimu ya uponyaji wake. Yule mwanamke alipogusa upindo wa vazi lake Kristo na kupona ugonjwa wake, Kristo alimwambia,"Imani yako imekuponya." (Math 9:22). Wote wanaweza kupata imani ya Yesu na uweza wa Roho Mtakatifu. Tunayo nguvu ya Roho Mtakatifu , ahadi tulivu ya imani ambayo inaweza kudai ahadi zake Mungu. Niwajibu wetu kuwakabidhi kwa Mungu wagonjwa na wale wanaoteseka kwa njia ya mikono ya imani yetu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni