Ijumaa, 5 Juni 2015

ADAMU WAWILI WAKUTANA:

Waliokombolewa walipokaribishwa ktk mji wa Mungu, kulikuwa na shangwe kuu. Adamu wawili karibu wakutana. Mwana wa Mungu atampokea baba wa taifa la kibinadamu, ambaye alimwumba,akatenda dhambi ambazo zilisababisha kusukubishwa kwa Mwokozi, na kupata akama ktk mwili wake. Adamu anapoona alama za misumari ktk mikono yake, anajitupa chini ya miguu ya Kristo. Mwokozi anamwinua na kumwambia atazame tena bustani ya Edeni, ambayo alifukuzwa kwa siku nyingi. Maisha ya Adamu yamekuwa ya huzuni nyingi. Kila mara alipoona majani yakinyauka na alipoua mnyama wa sadaka, iki ktmpatanisha na Mungu, yote hayo yalimktmbusha ubaya wa dhambi. Aliona uchungu wa ajabu, mambo hayo yote yakitupwa kwake, kwamba niyeye aliyesababisha, alijuta kabisa. Akafa ktk tumaini. Na sasa kwakuwa akisamehewa, amerudishiwa hali yake ya kwanza. Akijaa furaha tele, aliuona mti wa uzima uliokuwa chakula chake. Mwokozi anamwongoya kwenda kwemye mti wa uzima na akaambiwa ale matunda yake. Adamu aliona maeldu ya ukoo wake ambao wamekombolewa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni