Jumatatu, 1 Juni 2015

MAKAO YAKO KTK YERUSALEMU MPYA.

Kamwe ulimwengu haujapata kuona mji kama huu, usio na wahalifu, mabanda ya maskini, wala polisi. Mji huu unatajwa kuwa ni "mke wa Mwana Kondoo" na nimakao mazuri ya wale wanaomfuata mwana kondoo popote aendapo. Ni mji wa kweli na halisi, unaokaliwa na watu halisi. Utakuwa ni kutimiza tumaini ka Ibrahimu."Maana alikuwa akiutazamia mji wenye misingi, ambao mwenye kuubuni na kuujenga ni Mungu." Lakini sasa waitamani nchi iliyo bora, yaani, ya mbinguni. Kwahiyo Mungu haoni haya kuitwa Mungu wao, maana amewatengenezea mji" Ebr 11:10,16. Hakuna mojawapo ya miji ya ulimwengu huu ulio na msingi halisi, kwasababu yote itapita kama ilivyopita miji ya nyakati za Ibrahimu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni