Jumanne, 16 Juni 2015

UHUSIANO WETU NA SHERIA ZA MBINGUNI:

Sheria kuu zile zile zinazoongoza nyota na chembe ndogo sana (atom) huongoza pia maisha ya kibinadamu. Chanzo cha uhai wote ni Mungu. Kuivunja sheria yake, kimaumbile, kiakili, ama kimaadili, ni kujiweka mwenyewe kinyume na taratibu za Mungu ktk uumbaji wake wote, matokeo yake ni mafarakano, machafuko, na maangamizi. Juu ya viumbe vyake Mungu umewekwa wajibu mtakatifu wa: (1)Kutambua kwamba Mungu ndiye mwanzilishi wa sheria zote. (2)Kujifunza kuzielewa sheria za Mungu. (3)Kuzitumia sheria za Mungu ktk shughuli za kila siku za maisha yetu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni