Jumanne, 16 Juni 2015

IMANI KTK UWEZA WA MUNGU:

Yatupasa kushirikiana na Mungu ktk kuitunza miili yetu. Upendo kwa Mungu ni wamuhimu kwa uzima na afya yetu, ili kuwa na afya kamili, mioyo yetu haina budi kujazwa na upendo na tumaini na furaha ktk Bwana. Afya bora kuliko kuliko zote ya mwili, akili, na roho inaweza kupatikana tu kwa kuunganishwa na nguvu za Mungu. Kadiri afya kijumla inavyozidi kuwa bora, ndivyo uwezo wetu wa kumheshimu na kumtukuza muumbaji na mkombozi wa wanadamu utakavyozidi kuwa mkubwa zaidi kwa njia ya kuakisi tabia yake kwa ulimwengu huu. Muungano kati ya ubinadamu na uungu hutokea ktk sehemu ya mbele ya ubongo. Neva za ubongoni zinazowasiliana na mfumo mzima wa mwili ndiyo njia pekee ya mbingu ya kuweza kuwasiliana na mwanadamu na kuyabadilisha maisha yake ya ndani. Uweza wa Mungu unapoungana na maisha ya kibinadamu, unaathiri; (1)Uhusiano wetu na Mungu. (2)Uhusiano wetu na sheria za mbinguni.(3)Huduma yetu kwa Mungu. (4)Huduma yetu kwa wengine.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni