(1) Mungu ameahidi kutupatia hekima t
ukimwomba. (Yakobo 1:5).
(2)Chunguza Moyo wako uone kama Kuna dhambi yo yote iliyojificha au unayoijua inayoweza kumzuia Mungu kujibu maombi yako (Zaburi 66:18).
(3)Chunguza makusudi yako ili uone kama kile unachoomba ni Kwa utukufu was Mungu (Yakobo 4:3).
(4) Pamoja na kuamini kwamba Mungu anataka kukuongoza, amini pia kwamba atakuongoza (Zaburi 32:8; Isaya 58:11).
(5) Angalia kama Kuna kanuni zo zote katika Biblia zinazohusiana katika maamuzi unayotaka kuyafanya. Biblia ni hazina kuu ya maelekezo. Mara nyingi Mungu hutuongoza Kwa njia ya neno lake (Zaburi 119:10,11,105,133).
(6) Tafuta ushauri toka Kwa washauri wa Kikristo, ambao ni wacha Mungu, wanaoliamini neno la Mungu (Mith 11:14; 15:22).
(7) Angalia Majaliwa- mazingira yaliyoamriwa na Mungu yanayoonyesha njia unayopaswa kuifuata."Majaliwa" haya ni kama mabango yanayotusaidia, katika hatua za kufanya maamuzi. Hayawezi kuwa badala ya neno la Mungu, uamuzi timamu au akili ya kuzaliwa. Yanatusaidia katika hatua za kufanya maamuzi ( Mith 23:26; Mhubiri 8:5; Warumi 8:28).
(8) Ukishaomba Kwa dhati juu ya uamuzi fulani, umeangalia neno la Mungu linavyoshauri, umetafakari Kwa makini juu yake, umepata ushauri na kuangalia mwelekeo wa Majaliwa, fanya uamuzi wa busara kadri iwezekanavyo, ukiamini kwamba Mungu mwenyewe ndiye anayekuongoza (Zaburi 90:12).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni