Patakuwa na makundi mawili tu duniani, watoto watiifu wa Mungu na wale wasiotii. Siku moja Kristo aliweka mbele ya wasikilizaji wake kazi ile ya hukumu kwa maneno haya: "Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake, na mataifa yote watakusanyika mbele zake, naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi; atawaweka kondoo mkono wake wa kuume na mbuzi mkono wake wa kushoto. Kisha mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume. Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu; kwa maana nilikuwa na njaa mkanipa chakula, .................Mathayo 25:31-40. Kwa njia hiyo Kristo anayafungamanisha mambo yale yale ayapendayo pamoja na yale ya wanadamu wanaoteseka. Kila jambo wanalotendewa watoto wake analiangalia kama ametendewa yeye mwenyewe. Wale wanaodai kwamba wanao utakaso wa kisasa wangeweza kuja mbele yake wakijisifu na kusema, "Bwana, Bwana, hivi wewe hutujui sisi? Hatujafanya unabii kwa jina lako? na katika jina lako kutoa pepo? na katika jina lako kufanya miujiza mingi? Watu hao wanaoelezwa hapo , wanaotoa madai ya kinafiki, wakionekana kumweka Yesu katika mambo yao yote waliyofanya, nimfano halisi wa wale wanaodai kwamba wanao utakaso wa kisasa. Lakini wanaendelea kupiga vita sheria ya Mungu ( Amri Kumi). Kristo anawaita hao kuwa ni watenda maovu kwasababu hao ni wadanganyifu, wakiwawamejivika mavazi ya haki kuficha tabia zao zenye kasoro, yaani uovu ule walio nao ndani ya mioyo yao michafu. Shetani ameshuka chini katika siku hizi za mwisho akiwa na madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea. Kwa uweza wa fahari yake ya kishetani anafanya miujiza mbele ya macho ya manabii hao wa uongo, na mbele ya wanadamu, akidai kwamba yeye ni Kristo mwenyewe hasa. Shetani anawapa uwezo wake wale wanaomsaidia katika kuendeleza madanganyo yake; kwahiyo, wale wanaodai kuwa wanao uwezo mkubwa wa Mungu, wanaweza kutambuliwa tu kwa njia ya yule Mgunduzi Mkuu ( Msema Kweli), yaani,Sheria yake Yehova ( Amri Kumi)-Kutoka 20:3-17: Isaya 8:20. Bwana anatuambia sisi kwamba kama pangekuwa na uwezekano ( hao manabii wa uongo) wangeweza kuwadanganya yamkini hata walio wateule. Mavazi ya kondoo waliyojivika yanaonekana kuwa ni mavazi yao halisi, yaani, halisi kabisa kiasi kwamba mbwa mwitu huyo anaweza kutambuliwa tu kama sisi tutakwenda kuiangalia kanuni ile kuu ya Maadili ( Amri Kumi) na kuwagundua kuwa hao ni wavunjaji wa sheria ya Yehova ( Amri Kumi).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni