Tukiziungama dhambi zetu, yeye ni mwinifu na wahaki hata atuondolee dhambi zetu, nakutusafisha na udhalimu wote.(1Yohana1:9). Mungu anataka sisi tuziungame dhambi zetu na kuinyenyekeza mioyo yetu mbele zake. Lakini kwa wakati uo huo inatupasa kumwamini yeye kama Baba yetu mwenye huruma, ambaye hatawaacha wale wanaomtumainia. Wengi wetu tunatembea kwa kuona si kwa imani. Tunayaamini mambo yale yanayoonekana, lakini hatuzithamini ahadi zake za thamani zilizotolewa kwetu katika neno la Mungu, na hata hivyo , hatuwezi kumvunjia Mungu heshima kwa dhahiri kuliko kujionjesha kwake kuwa sisi hatuyaini yale asemayo kwetu, na kwamba tuna mashaka iwapo Bwana anasema kweli kwetu ama anatudanganya. Mungu hatuachi kwasababu ya dhambi zetu. Twaweza kufanya makosa(dhambi) na kumhuzunisha Roho wake. Lakini tunapotubu na kuja kwake na mioyo iliyopondeka yeye hawezi kukataa kutupokea. Kuna vipingamizi vinavyopaswa kuondolewa (1) Hisia mbaya (2) Kiburi (3) roho ya kujitosheleza (4) kukosa uvumilivu na manung'uniko. Hayo yote yanatutenga na Mungu.
Dhambi hazina budi kuungamwa, yatupasa pawepo kazi kubwa yenye kina ya neema moyoni. Wale wanaojiona dhaifu na waliokata tamaa waweza kuwa watu wa Mungu wenye nguvu, na kufanya kazi bora kwa Bwana. Wakati Bwana alipowaruhusu nyoka wenye sumu kuwauma Waisraeli walioasi, Musa aliagizwa kuinua nyoka wa shaba nyeupe, na kuwaamuru wote waliojeruhiwa kumwangalia ili wapate kupona. Lakini wengi hawakuona msaada katika dawa hii iliyoamriwa na Mungu. Maiti na watu waluokuwa katika hali ya kufa walizunguka pande zote, nao wakajua hakika pasipo msaada wa Mungu watakufa hakika; Lakini walilia na kuomboleza kwa sababu ya majeraha yao, maumivu yao, mauti yao mpaka wameishiwa na nguvu zao, na macho yao yakageuka kama mtu aliyekufa, wakati ambapo wangeweza kuponywa mara moja kama wangemtazama yule nyoka. "Kama Musa alivyomwinua yule nyoka jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa; ili kila mtu amwaminiye awe na uzima wa milele katika Yeye." Kama unafahamu dhambi zako, usizitumie nguvu zako zote kuomboleza juu yake, bali tazama upate kuponywa. Yesu ndiye Mwokozi wetu peke yake; na ijapokuwa mamilioni wenye kuhitaji kuponywa watakataa rehema yake iliyotolewa, hakuna mtu ambaye ataamini sifa njema za Kristo atakaye achwa apotee. Kwa kuwa tunajua kwamba bila Kristo maishani tu wadhaifu sana, hatupaswi kukata tamaa, inatupasa kumtegemea Mwokozi aliyesulubiwa na kufufuka. Jipe moyo maskini, mgonjwa wa dhambi, uliye kata tamaa, tazama upate kuponywa. Yesu ameahidi katika neno lake ya kuwa atawaokoa wote wanaomwendea. Njoo kwa Yesu upate pumziko na amani. Unaweza upate mbaraka hata sasa.
Jumanne, 31 Mei 2016
KRISTO NI HAKI YETU
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni