Jumatatu, 16 Novemba 2020

YESU ANADAI HESHIMA.




Yesu alipokuwa amepita upeo wa macho ya wanafunzi wake pale juu ya mlima Mizeituni, alilakiwa na Jeshi la Mbinguni, ambalo, huku likiimba nyimbo za furaha na ushindi, lilimsindikiza akienda juu.
Katika malango ya mji wa Mungu majeshi ya malaika wengi wasiohesabika  walikuwa wakimngojea. Kama Krsto alivyokaribia hayo malango wale malaika waliokuwa wakija naye, katika sauti ya ushindi waliwaambia wale malaika waliokuwa pale malangoni:
             Inueni vichwa vyenu enyi malango, inukeni enyi malango ya milele, Mfalme wa utukufu apate kuingia.
Wale malaika waliokuwa wakingojea pale katika malango wakauliza:
Ninani  Mfalme wa utukufu?
Kuuliza hivi si kwamba hawajui, ila walitamani kulisikia hilojibu la sofa ya ajabu.
Bwana mwenye nguvu, hodari. Bwana hodari wa Vita. Inueni vichwa vyenu enyi malango, naam, viinueni enyi malango ya milele. Mfalme wa utukufu apate kuingia.
Wakauliza tena:  Ninani huyu Mfalme wa utukufu?
Wakajibiwa: Bwana wa majeshi, true ndiye Mfalme wa utukufu.
Ndipo yale malango ya mji yakafunguliwa wazi na lile jeshi kubwa la Malaika likaingia kupitia malango hayo, huku wakiimba Kwa furaha na upeo.