Jumatano, 8 Februari 2017

WATENDAKAZI PAMOJA NA MUNGU.

Fungi kuu: Mithali 3:9,10/11:24 & Isa 32:8  Hekima ya Mungu imeonyeshwa katika mpango wa wokovu, sheria ya kutenda na wajibu, inafanya kazi kwa ukarimu katika sehemu zake zote, kubarikiwa maradufu. Anayetoa kwa wahitaji anawabariki wengine na kujibarikia mwenyewe katika mibaraka ya hali ya juu.               


UTUKUFU WA INJILI:                       Ili yakwamba mwanadamu asipoteze mibaraka ya matokeo ya ukarimu, Mwokozi wetu alianzisha mpango wa kumhesabu kama mtendakazi wake. Mungu angaliweza kuendesha kusudi lake la kuwaokoa wenye dhambi pasipo msaada wa mwanadamu; lakini alifahamu kwamba mwanadamu asingefurahi kukosa na sehemu ya kufanya katika kazi hii kubwa. Kwa mnyororo wa mambo ambayo yangevuta mapenzi take alitoa kwa mwanadamu njia zilizobora za kustawisha ukarimu, na kumfanya awe na tabia ya utoaji kwa kuwasaidia masikini na kwa kuendesha mbele kazi yake.  Ni utukufu wa injili ulioanzishwa juu ya Kanuni ya kulirudisha taifa  lililoanguka katika mfano wa Mungu kwa njia ya utoaji wa ukarimu. Kazi hii ilianza katika makao ya mbinguni. Kule mbinguni  Mungu alitoa kwa mwanadamu upendo ulio wazi wazi (Yohana 3:16). Moyo wa ukarimu ni moyo wa mbinguni. Dhabihu ya upendo wa Kristo ilionyeshwa msalabani. Ili mwanadamu spate kuokolewa, alitoa yote aliyokuwa nayo, na ndipo akajitoa mwenyewe.           

MIBARAKA YA UWAKILI:                   Katika agizo kwa wanafunzi wake,  "Enendeni ulimwenguni mwote mkaihubiri injili kwa kila kiumbe,"   Kristo aliwapa kazi ya kueneza ujuzi wa neema yake,. Maadamu wengine wakienda kuhubiri, huwaita wengine kufanya wajibu wao kwa kutoa sadaka ambayo itasaidia kuendesha kazi yake  duniani.  Kila kitu chema kiliwekwa hapa duniani na mkono wa ukarimu wa Mungu kama kielelezo cha upendo wake kwa mwanadamu. Masikini ni wake na kazi ya injili ni yake. Fedha na dhahabu ni Mali ya Mungu, na angaliweza kuzileta kutoka mbinguni kama angalitaka. Lakini badala yake alimfanya mwanadamu kuwa wakili wake kwa kumkabidhi fedha, sio kukusanya, lakini kuzitumia kwa kuwasaidia wengine. Kwa hiyo amemweka mwanadamu kuwa njia ambayo atagawanyia mibaraka yake duniani.                                  Upendo  uliofunuliwa Kalwari ungalionyeshwa na kuimarishwa kwa kuenezwa miongoni mwa makanisa yetu.                        Kutana kando ya msalaba wa Kalwari katika kujikana nafsi na kwa kujinyima. Mungu atakubariki ukitimiza wajibu wako. Unapokaribia kiti cha neema unapojiona kwamba umeunganishwa kwa kiti cha enzi mnyororo uliotoka  mbinguni mpaka duniani, kuwatoa watu kutoka katika shimo la dhambi, ndipo moyo wako utakuwa na upendo kwa ndugu na Dada zako ambao hawana Mungu wala tumaini katika ulimwengu.(9T 253-256).Hakuna maoni:

Chapisha Maoni